Ezekiel 26:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakuteremsha shimoni ili ujiunge na walioko huko, walioishi duniani zamani; nitakufanya ukae huko katika mahame milele. Hutakaliwa na watu milele na hutakuwa na nafasi miongoni mwa nchi za walio hai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale wanaoshuka shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale wanaoshuka shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakuteremsha shimoni ili ujiunge na walioko huko, walioishi duniani zamani; nitakufanya ukae huko katika mahame milele. Hutakaliwa na watu milele na hutakuwa na nafasi miongoni mwa nchi za walio hai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale washukao shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale washukao shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale washukao shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale washukao shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakuteremsha shimoni ili ujiunge na walioko huko, walioishi duniani zamani; nitakufanya ukae huko katika mahame milele. Hutakaliwa na watu milele na hutakuwa na nafasi miongoni mwa nchi za walio hai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, nitakapokusukuma, ushuke kwao walioshuka shimoni, kwao watu wa kale, ndipo nitakapokukalisha kuzimuni chini ya nchi kwenye mabomoko ya kale kwao washukao shimoni, kusudi watu wasikae mwako tena. Lakini nchi yao walio wazima nitaipitia urembo mwingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakuteremusha ndani ya shimo kusudi ujiunge na wale wanaokuwa huko, walioishi zamani katika dunia; utakaa kule katika matongo kwa milele. Hautakaliwa na watu milele na hautakuwa na nafasi katika inchi za wanaokuwa wazima.