Ezekiel 27:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walichukua mialoni toka Bashani wakakuchongea makasia yako; walikitengenezea silaha kwa misonobari ya kisiwa cha Kupro, na kuipamba kwa pembe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walichukua mialoni kutoka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha yako na kuipamba kwa pembe za ndovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walichukua mialoni toka Bashani wakakuchongea makasia yako; walikitengenezea silaha kwa misonobari ya kisiwa cha Kupro, na kuipamba kwa pembe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walichukua mialoni toka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha yako na kuipamba kwa pembe za ndovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walichukua mialoni toka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha yako na kuipamba kwa pembe za ndovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walichukua mialoni toka Bashani wakakuchongea makasia yako; walikitengenezea silaha kwa misonobari ya kisiwa cha Kupro, na kuipamba kwa pembe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mivule ya Basani waliitumia ya kukufanyizia makasia, vyumba vyako walivifanya kwa mbao za misagawi zilizopangiliwa kwa meno ya tembo, zilizotoka visiwani kwa Wakiti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walitwaa miti ya mialo toka Basani wakakuchongea makasia; walikutengenezea mbao za kuikalia kwa miti ya misunobari ya kisanga cha Kipuro, na kuipamba kwa pembe ya tembo.