Ezekiel 27:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazee wa Gebali na mafundi wao walikuwa kwako kuziba nyufa zako. Mabaharia waliokuwa wakipitia kwako walifanya biashara nawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wazee wa Gebali pamoja na mafundi stadi walikuwa mafundi wako kwenye meli. Meli zote za baharini na mabaharia wao walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wazee wa Gebali na wenye akili wake walikuwa ndani yako, wenye kutia kalafati; merikebu zote za bahari na mabaharia wao walikuwa ndani yako, ili kubadiliana biashara yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazee wa Gebali na mafundi wao walikuwa kwako kuziba nyufa zako. Mabaharia waliokuwa wakipitia kwako walifanya biashara nawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wazee wa Gebali pamoja na mafundi stadi walikuwa mafundi wako melini. Meli zote za baharini na mabaharia wao walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wazee wa Gebali pamoja na mafundi stadi walikuwa mafundi wako melini. Meli zote za baharini na mabaharia wao walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wazee wa Gebali na wenye akili wake walikuwa ndani yako, wenye kutia kalafati; merikebu zote za bahari na mabaharia wao walikuwa ndani yako, ili kubadilishana biashara yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazee wa Gebali na mafundi wao walikuwa kwako kuziba nyufa zako. Mabaharia waliokuwa wakipitia kwako walifanya biashara nawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wazee wa Gebali na mafundi wake walikuwa kwako wa kuziziba nyufa zako. Merikebu zote za baharini zikafika kwako na mabaharia wao, wakauziana na wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wazee wa Gebali na wenye akili wake walikuwa ndani yako, wenye kutia kalafati; merikebu zote za bahari na mabaharia wao walikuwa ndani yako, ili kubadiliana biashara yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazee wa Gebali na wafundi wao walikuwa wakiziba nyufa zako. Wachuuzi wa bahari waliokuwa wakipitia kwako walifanya biashara nawe.