Ezekiel 28:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimteua malaika kukulinda, uliishi katika mlima wangu mtakatifu na kutembea juu ya vito vinavyometameta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulipakwa mafuta kuwa kerubi mlinzi, kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu. Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu; ulitembea katikati ya vito vya moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimteua malaika kukulinda, uliishi katika mlima wangu mtakatifu na kutembea juu ya vito vinavyometameta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi, kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokusimika. Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu; ulitembea katikati ya mawe ya moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi, kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu. Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu; ulitembea katikati ya vito vya moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nilikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huku na huko kati ya mawe ya moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilimteua malaika kukulinda, uliishi katika mlima wangu mtakatifu na kutembea juu ya vito vinavyometameta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukawa kama Kerubi aliyepakwa mafuta kuwa mlinzi, nikakuweka juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, ukawako ukitembea katika mawe yenye moto katikati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilichagua kerubi kwa kukulinda, uliishi katika mulima wangu mutakatifu na kutembea juu ya mawe yanayometameta.