Ezekiel 28:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ufanisi wa biashara yako ulikujaza dhuluma, ukatenda dhambi. Kwa hiyo nilikufukuza kama kinyaa, mbali na mlima wangu mtakatifu. Na yule malaika aliyekulinda akakufukuzia mbali na vito vinavyometameta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutokana na biashara yako iliyoenea, ulijazwa na dhuluma, nawe ukatenda dhambi. Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu, nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi, kutoka katikati ya vito vya moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ufanisi wa biashara yako ulikujaza dhuluma, ukatenda dhambi. Kwa hiyo nilikufukuza kama kinyaa, mbali na mlima wangu mtakatifu. Na yule malaika aliyekulinda akakufukuzia mbali na vito vinavyometameta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutokana na biashara yako iliyoenea, ulijazwa na dhuluma nawe ukatenda dhambi. Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka katika mlima wa Mungu, nami nikakufukuza, Ee kerubi mlinzi, kutoka katikati ya mawe ya moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutokana na biashara yako iliyoenea, ulijazwa na dhuluma, nawe ukatenda dhambi. Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu, nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi, kutoka katikati ya vito vya moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ufanisi wa biashara yako ulikujaza dhuluma, ukatenda dhambi. Kwa hiyo nilikufukuza kama kinyaa, mbali na mlima wangu mtakatifu. Na yule malaika aliyekulinda akakufukuzia mbali na vito vinavyometameta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa uchuuzi wako mwingi ukajaa makorofi ndani yako, ukakosa, nami nikakukimbiza kwenye mlima wa Mungu, kwa kuwa ulijipatia uchafu, nikakutowesha uliyekuwa kama Kerubi alindaye, uondoke katika yale mawe yenye moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ustawi wa biashara yako ulikujaza ukali, ukatenda zambi. Kwa hiyo nilikufukuza kama muchafu, mbali na mulima wangu mutakatifu. Na yule kerubi aliyekulinda akakufukuzia mbali na mawe yanayometameta.