Ezekiel 28:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe mtu! Mwambie mfalme wa Tiro kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe una kiburi cha moyo, na umesema kwamba wewe ni mungu, kwamba umekalia kiti cha enzi cha miungu, umekaa mbali huko baharini. Lakini, wewe ni binadamu tu wala si Mungu, ingawa wajiona kuwa una hekima kama Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna na umesema, “Mimi ni mungu; nami ninaketi kwenye kiti cha enzi cha mungu katika moyo wa bahari.” Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu, ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe mtu! Mwambie mfalme wa Tiro kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe una kiburi cha moyo, na umesema kwamba wewe ni mungu, kwamba umekalia kiti cha enzi cha miungu, umekaa mbali huko baharini. Lakini, wewe ni binadamu tu wala si Mungu, ingawa wajiona kuwa una hekima kama Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: “ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna na umesema, “Mimi ni mungu; nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu katika moyo wa bahari.” Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu, ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna na umesema, “Mimi ni mungu; nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu katika moyo wa bahari.” Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu, ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe mtu! Mwambie mfalme wa Tiro kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wewe una kiburi cha moyo, na umesema kwamba wewe ni mungu, kwamba umekalia kiti cha enzi cha miungu, umekaa mbali huko baharini. Lakini, wewe ni binadamu tu wala si Mungu, ingawa wajiona kuwa una hekima kama Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu, mwambie mfalme wa Tiro: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Moyo wako umejikuza kwamba: Mungu ni mimi, tena ninakaa pake Mungu baharini katikati! Kumbe nawe u mtu, hu Mungu, nawe moyo wako ukajiwazia kuwa kama moyo wa Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe mwanadamu! Umwambie mufalme wa Tiro kwamba Bwana wenu Yawe anasema hivi: Wewe una kiburi cha moyo, na umesema kwamba wewe ni mungu, kwamba umeikalia kiti cha kifalme cha miungu, umekaa mbali huko katika bahari. Lakini, wewe ni mutu tu wala si mungu, ingawa unajiona kuwa na hekima kama mungu.