Ezekiel 28:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu asema, “Mataifa jirani na Waisraeli ambayo yalikuwa yanawaudhi hayataweza tena kuwaumiza Waisraeli kama vile kwa miiba na michongoma. Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru, wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hautakuwapo mchongoma uchomao kwa nyumba ya Israeli; wala mwiba uumizao miongoni mwa wote wamzungukao, waliowatenda mambo ya jeuri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu asema, “Mataifa jirani na Waisraeli ambayo yalikuwa yanawaudhi hayataweza tena kuwaumiza Waisraeli kama vile kwa miiba na michongoma. Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hautakuwapo mchongoma uchomao nyumba ya Israeli; wala mwiba uumizao miongoni mwa wote wamzungukao, waliowatenda mambo ya jeuri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu asema, “Mataifa jirani na Waisraeli ambayo yalikuwa yanawaudhi hayataweza tena kuwaumiza Waisraeli kama vile kwa miiba na michongoma. Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mlango wa Isiraeli hautaona tena miiba ya kuwachoma wala machomo ya kuwaumiza kwao wote wanaokaa na kuwazunguka waliowabeza; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hautakuwapo mchongoma uchomao kwa nyumba ya Israeli; wala mwiba uumizao miongoni mwa wote wamzungukao, waliowatenda mambo ya jeuri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu anasema: Mataifa jirani za Waisraeli ambayo yalikuwa yanawauzi hayataweza tena kuwaumiza Waisraeli kama vile kwa miiba na michongoma. Halafu watajua kwamba mimi ni Bwana wao Yawe.