Ezekiel 28:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya na kuwaleta Waisraeli kutoka katika mataifa yote ambamo walitawanywa. Hivyo nitawafanya watu wa mataifa waone kuwa mimi ni mtakatifu. Watu wa Israeli wataishi katika nchi yao ambayo mimi nilimpa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao wametawanyika kati yao, na kutakasika kati yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu, Yakobo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya na kuwaleta Waisraeli kutoka katika mataifa yote ambamo walitawanywa. Hivyo nitawafanya watu wa mataifa waone kuwa mimi ni mtakatifu. Watu wa Israeli wataishi katika nchi yao ambayo mimi nilimpa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka katika mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao wametawanyika kati yao, na kutakasika kati yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu, Yakobo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawakusanya na kuwaleta Waisraeli kutoka katika mataifa yote ambamo walitawanywa. Hivyo nitawafanya watu wa mataifa waone kuwa mimi ni mtakatifu. Watu wa Israeli wataishi katika nchi yao ambayo mimi nilimpa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitakapowakusanya walio ukoo wa Isiraeli na kuwatoa kwenye makabila yote, walikotawanyikia, ndipo, nitakapoutokeza kwao utakatifu wangu, wao wa mataifa wauone; nao watakaa katika nchi yao, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao wametawanyika kati yao, na kutakasika kati yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu, Yakobo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitawakusanya na kuwaleta Waisraeli kutoka katika mataifa yote ambamo walisambazwa. Hivyo nitawafanya watu wa mataifa waone kwamba mimi ni mutakatifu. Waisraeli wataishi katika inchi yao ambayo mimi nilimupa mutumishi wangu Yakobo.