Ezekiel 29:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kati ya miji yote iliyoharibiwa, miji ya Misri itakuwa mitupu kwa miaka arubaini. Nitawatawanya Wamisri kati ya watu wa mataifa mengine na kuwasambaza katika nchi nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwatapanya katika nchi nyingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arobaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kati ya miji yote iliyoharibiwa, miji ya Misri itakuwa mitupu kwa miaka arubaini. Nitawatawanya Wamisri kati ya watu wa mataifa mengine na kuwasambaza katika nchi nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huko na huko katika nchi nyingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi nyingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arobaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kati ya miji yote iliyoharibiwa, miji ya Misri itakuwa mitupu kwa miaka arubaini. Nitawatawanya Wamisri kati ya watu wa mataifa mengine na kuwasambaza katika nchi nyingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitaitoa nchi ya Misri kuwa peke yake katikati ya nchi nyingine zilizo peke yao nazo, nayo miji yake itakuwa peke yao katikati ya miji mingine iliyo mabomoko tu, itakuwa hivyo miaka 40. Nao Wamisri nitawatawanya kwenye mataifa mengine na kuwatupatupa katika nchi zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arobaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati ya miji yote iliyoharibika, miji ya Misri itakuwa mitupu kwa miaka makumi ine. Nitawasambaza Wamisri kati ya watu wa mataifa mengine na kuwaeneza katika inchi zingine.