Ezekiel 29:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakutupa jangwani, wewe na samaki hao wote. Mwili wako utaanguka mbugani; wala hakuna atakayekuokota akuzike. Nimeutoa mwili wako uwe chakula cha wanyama wakali na ndege.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitakutupa jangwani, wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako. Utaanguka uwanjani, nawe hutakusanywa au kuchukuliwa. Nitakutoa uwe chakula kwa wanyama wa nchi na ndege wa angani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitakuacha hali umetupwa jangwani, wewe na samaki wote wa mito yako; utaanguka juu ya uso wa uwanda; hutakusanywa, wala kuwekwa pamoja; nimekutoa uwe chakula cha wanyama wa nchi, na cha ndege wa angani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakutupa jangwani, wewe na samaki hao wote. Mwili wako utaanguka mbugani; wala hakuna atakayekuokota akuzike. Nimeutoa mwili wako uwe chakula cha wanyama wakali na ndege.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitakutupa jangwani, wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako. Utaanguka uwanjani, nawe hutakusanywa au kuchukuliwa. Nitakutoa uwe chakula kwa wanyama wa nchi na ndege wa angani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitakutupa jangwani, wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako. Utaanguka uwanjani, nawe hutakusanywa au kuchukuliwa. Nitakutoa uwe chakula kwa wanyama wa nchi na ndege wa angani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitakuacha ukiwa umetupwa jangwani, wewe na samaki wote wa mito yako; utaanguka katika uwanda ulio wazi; hutakusanywa, wala kuwekwa pamoja; nimekutoa uwe chakula cha wanyama wa nchi, na cha ndege wa angani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakutupa jangwani, wewe na samaki hao wote. Mwili wako utaanguka mbugani; wala hakuna atakayekuokota akuzike. Nimeutoa mwili wako uwe chakula cha wanyama wakali na ndege.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nitakubwaga nyikani wewe pamoja na samaki wote waliokuwamo majitoni mwako, hutaokotwa wala hutakusanywa, ila nitakutoa, nyama wa porini na ndege wa angani wakule.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitakuacha hali umetupwa jangwani, wewe na samaki wote wa mito yako; utaanguka juu ya uso wa uwanda; hutakusanywa, wala kuwekwa pamoja; nimekutoa uwe chakula cha wanyama wa nchi, na cha ndege wa angani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakutupa katika jangwa, wewe na samaki hao wote. Mwili wako utaangukia katika mbuga; wala hakuna atakayekuokota kusudi akuzike. Nimeutoa mwili wako ukuwe chakula cha nyama wakali na ndege.