Ezekiel 29:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu umesema kuwa mto Nili ni wako, kwamba ndiwe uliyeufanya, basi, nchi yako, Misri, itakuwa tupu na jangwa. Ndipo watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. “ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliuumba,”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu umesema kuwa mto Nili ni wako, kwamba ndiwe uliyeufanya, basi, nchi yako, Misri, itakuwa tupu na jangwa. Ndipo watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA. “ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Nile ni wangu; mimi niliufanya,”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi bwana. “ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliufanya,”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu umesema kuwa mto Nili ni wako, kwamba ndiwe uliyeufanya, basi, nchi yako, Misri, itakuwa tupu na jangwa. Ndipo watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, nchi ya Misri itakapokuwa peke yake kwa kuharibiwa, ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, kwa kuwa alisema: Jito ni langu, mimi ndiye aliyelifanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu umesema kwamba muto Nili ni wako, kwamba ndiwe uliyeufanya, basi, inchi yako, Misri, itakuwa tupu na jangwa. Halafu watu watatambua kwamba mimi ni Yawe.