Ezekiel 3:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikimwambia mtu mwovu kwamba hakika atakufa, nawe humwonyi au kumwambia aache njia yake potovu ili kuyaokoa maisha yake, basi, mtu huyo mwovu atakufa kwa uovu wake; lakini damu yake nitakudai wewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ na wewe usimwonye mtu huyo au kumshauri aache njia zake mbaya ili kuokoa maisha yake, huyo mtu mwovu akifa katika dhambi yake, damu yake nitaidai mkononi mwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikimwambia mtu mwovu kwamba hakika atakufa, nawe humwonyi au kumwambia aache njia yake potovu ili kuyaokoa maisha yake, basi, mtu huyo mwovu atakufa kwa uovu wake; lakini damu yake nitakudai wewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ na wewe usipomwonya mtu huyo au kumshauri aache njia zake mbaya ili kuokoa maisha yake, huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake na damu yake nitaidai mkononi mwako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ na wewe usipomwonya mtu huyo au kumshauri aache njia zake mbaya ili kuokoa maisha yake, huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake na damu yake nitaidai mkononi mwako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikimwambia mtu mwovu, Hakika utakufa; na wewe usimpe maonyo, wala kusema na huyo mtu mwovu ili kumwonya, ili kusudi aache njia yake mbaya na kuiokoa roho yake; mtu yule mwovu atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikimwambia mtu mwovu kwamba hakika atakufa, nawe humwonyi au kumwambia aache njia yake potovu ili kuyaokoa maisha yake, basi, mtu huyo mwovu atakufa kwa uovu wake; lakini damu yake nitakudai wewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninapomwambia mtu asiyenicha: Utakufa, nawe usipomwonya, usiposema naye yeye asiyenicha, kwamba umwonye, aiache njia yake, umpatie kuwapo uzimani, basi, yeye asiyenicha atakufa kwa manza zake, alizozikora, lakini damu yake nitakulipisha, kwani itakuwa imeishika mikono yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikimwambia mutu mwovu kwamba hakika atakufa, nawe haumwonyi au kumwambia aache mwenendo wake mubaya apate kuyaokoa maisha yake, basi, mutu huyo mwovu atakufa kwa uovu wake; lakini wewe utabeba lazima ya damu yake.