Ezekiel 3:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nguvu ya Mwenyezi-Mungu ilikuwa juu yangu; naye akaniambia, “Inuka uende mpaka sehemu tambarare nami nitaongea nawe huko.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yangu huko, naye akaniambia, “Simama uende sehemu tambarare, nami nitasema nawe huko.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mkono wa Bwana ulikuwako juu yangu huko; akaniambia, Ondoka, enenda uwandani; nami nitasema nawe huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nguvu ya Mwenyezi-Mungu ilikuwa juu yangu; naye akaniambia, “Inuka uende mpaka sehemu tambarare nami nitaongea nawe huko.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu huko, naye akaniambia, “Simama uende mpaka sehemu tambarare, nami nitasema nawe huko.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkono wa bwana ulikuwa juu yangu huko, naye akaniambia, “Simama uende mpaka sehemu tambarare, nami nitasema nawe huko.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mkono wa BWANA ulikuwako juu yangu huko; akaniambia, Ondoka, nenda bondeni; nami nitasema nawe huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nguvu ya Mwenyezi-Mungu ilikuwa juu yangu; naye akaniambia, “Inuka uende mpaka sehemu tambarare nami nitaongea nawe huko.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mkono wa Bwana ulipokuja kuwa juu yangu, akaniambia: Ondoka kwenda kwenye mbuga iliyoko bondeni! Ndiko, nitakakosema na wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mkono wa BWANA ulikuwako juu yangu huko; akaniambia, Ondoka, enenda uwandani; nami nitasema nawe huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akanijaza uwezo wake; naye akaniambia: Simama, uende katika bonde nami nitaongea nawe huko.