Ezekiel 3:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nikainuka na kwenda sehemu tambarare. Lo! Nikiwa huko nikauona utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukiwa umesimama huko kama utukufu ule niliokuwa nimeuona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo niliinuka nikaenda mahali tambarare. Utukufu wa Mwenyezi Mungu ulikuwa umesimama huko, kama utukufu ule niliouona kando ya Mto Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, nikaondoka, nikaenda uwandani, na tazama, utukufu wa Bwana ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nikainuka na kwenda sehemu tambarare. Lo! Nikiwa huko nikauona utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukiwa umesimama huko kama utukufu ule niliokuwa nimeuona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo niliinuka nikaenda mpaka mahali pa tambarare. Utukufu wa BWANA ulikuwa umesimama huko, kama utukufu ule niliouona kando ya Mto Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo niliinuka nikaenda mpaka mahali pa tambarare. Utukufu wa bwana ulikuwa umesimama huko, kama utukufu ule niliouona kando ya Mto Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, nikaondoka, nikaenda bondeni, na tazama, utukufu wa BWANA ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nikainuka na kwenda sehemu tambarare. Lo! Nikiwa huko nikauona utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukiwa umesimama huko kama utukufu ule niliokuwa nimeuona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaondoka kwenda kwenye mbuga iliyoko bondeni, mara nikauona utukufu wa Bwana, ukisimama hapo, ulikuwa kama ule utukufu, niliouona kwenye mto wa Kebari, nikaanguka kifudifudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, nikaondoka, nikaenda uwandani, na tazama, utukufu wa BWANA ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, nikasimama na kwenda katika bonde. Nikiwa huko nikauona utukufu wa Yawe ukiwa umesimama huko kama utukufu ule niliokuwa nimeuona karibu na muto Kebari; nami nikaanguka uso mpaka chini.