Ezekiel 30:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaukausha mto Nili na vijito vyake, na kuwauzia watu waovu nchi ya Misri. Nitasababisha uharibifu nchini kote kwa mkono wa watu wageni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitakausha vijito vya Mto Naili, na kuiuza nchi kwa watu waovu; kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilicho ndani yake. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena haya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi, Bwana, nimenena neno hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaukausha mto Nili na vijito vyake, na kuwauzia watu waovu nchi ya Misri. Nitasababisha uharibifu nchini kote kwa mkono wa watu wageni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitakausha vijito vya Nile na nitaiuza nchi kwa watu waovu, kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilichomo ndani yake. Mimi BWANA nimenena haya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitakausha vijito vya Naili na nitaiuza nchi kwa watu waovu, kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu kilichomo ndani yake. Mimi bwana nimenena haya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi, BWANA, nimenena neno hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaukausha mto Nili na vijito vyake, na kuwauzia watu waovu nchi ya Misri. Nitasababisha uharibifu nchini kote kwa mkono wa watu wageni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo majito yake nitayakausha, nayo nchi hiyo nitaiuza mikononi mwa watu wabaya, niiangamize kwa mikono ya wageni pamoja nayo yote yaliyomo. Mimi Bwana nimeyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi, BWANA, nimenena neno hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaukausha muto Nili na vijito vyake, na kuuzisha inchi ya Misri katika mikono ya watu waovu. Nitasababisha uharibifu katika inchi yote kwa mukono wa watu wageni. Ni Mimi Yawe ninayesema hivyo.