Ezekiel 30:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitaharibu vinyago vya miungu, na kukomesha sanamu mjini Memfisi. Hakutakuwa na mkuu tena huko Misri. Nitasababisha hofu itawale nchini Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi. Hapatakuwa tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu, wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri, nami nitatia hofu katika nchi ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitaharibu vinyago vya miungu, na kukomesha sanamu mjini Memfisi. Hakutakuwa na mkuu tena huko Misri. Nitasababisha hofu itawale nchini Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi. Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitaangamiza sanamu na kukomesha vinyago katika Memfisi Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri, nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu, wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri, nami nitatia hofu katika nchi ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitaharibu vinyago vya miungu, na kukomesha sanamu mjini Memfisi. Hakutakuwa na mkuu tena huko Misri. Nitasababisha hofu itawale nchini Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitayapoteza magogo ya kutambikia mle Nofu, hata vinyago nitavikomesha, pasiwe tena mkuu atokaye katika nchi ya Misri, tena nitaitisha nchi ya Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana MUNGU asema hivi; Pia nitaviharibu vinyago, nami nitavikomesha vitu vya ubatili katika Nofu, wala hapatakuwa na mkuu tena atokaye katika nchi ya Misri, nami nitatia hofu katika nchi ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitaharibu sanamu za miungu, na kukomesha miungu ya uongo ya muji wa Nofi. Hakutakuwa mukubwa tena huko Misri. Nitasababisha hofu itawale katika inchi ya Misri.