Ezekiel 30:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaiwasha moto nchi ya Misri. Pelusiumu utashikwa na dhiki kubwa, ukuta wa Thebesi utabomolewa, nao Memfisi utakabiliwa na adui mchana wazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitatia moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, na No itavunjika kabisa; na Nofu itakuwa na adui wakati wa mchana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaiwasha moto nchi ya Misri. Pelusiumu utashikwa na dhiki kubwa, ukuta wa Thebesi utabomolewa, nao Memfisi utakabiliwa na adui mchana wazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitaitia moto nchi ya Misri; Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. Thebesi itachukuliwa na tufani, Memfisi itakuwa katika taabu daima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitatia moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, na Tebesi itavunjika kabisa; na Nofu itakuwa na adui wakati wa mchana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaiwasha moto nchi ya Misri. Pelusiumu utashikwa na dhiki kubwa, ukuta wa Thebesi utabomolewa, nao Memfisi utakabiliwa na adui mchana wazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawasha moto katika Misri: Sini utaona machungu makuu, No utavunjwa kwa kubomolewa, Nofu utapata wanaousonga mchana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitatia moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, na No itavunjika kabisa; na Nofu itakuwa na adui wakati wa mchana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitateketeza inchi ya Misri kwa moto. Sini utashikwa na wasiwasi mukubwa, ukuta wa Nofi utabomolewa, nao Nofi utashambuliwa na waadui muchana wazi.