Ezekiel 30:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe mtu! Nimeuvunja mkono wa Farao mfalme wa Misri, nao haukufungwa ili uweze kupona na kuweza kushika upanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri, na tazama, haukufungwa ili kuutia dawa, haukuzongwa kwa kitambaa, upate kuwa na nguvu za kushika upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe mtu! Nimeuvunja mkono wa Farao mfalme wa Misri, nao haukufungwa ili uweze kupona na kuweza kushika upanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri, na tazama, haukufungwa ili kuutia dawa, haukuzongwa kwa kitambaa, upate kuwa na nguvu za kushika upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe mtu! Nimeuvunja mkono wa Farao mfalme wa Misri, nao haukufungwa ili uweze kupona na kuweza kushika upanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu, mkono wa Farao, mfalme wa Misri, nimeuvunja, lakini tazama, haukufungwa, upate kupona, hawakuutakia kitambaa tu, kwamba waufunge, wautie nguvu tena, upate kushika upanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri, na tazama, haukufungwa ili kuutia dawa, haukuzongwa kwa kitambaa, upate kuwa na nguvu za kushika upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe mwanadamu! Nimeuvunja mukono wa Mufalme wa Misri, nao haukutunzwa na dawa kusudi uweze kupona na kuweza kushika upanga.