Ezekiel 30:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vita vitazuka dhidi ya Misri, na wasiwasi mkuu utaikumba nchi ya Kushi, wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa, mali zao zitakapochukuliwa, na misingi ya miji yao kubomolewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Kushi. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na upanga utakuja juu ya Misri, na dhiki itakuwa katika Kushi, watakapoanguka watu waliouawa katika Misri, nao watauondoa wingi wa watu wake, na misingi yake itabomolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vita vitazuka dhidi ya Misri, na wasiwasi mkuu utaikumba nchi ya Kushi, wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa, mali zao zitakapochukuliwa, na misingi ya miji yao kubomolewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na upanga utakuja juu ya Misri, na dhiki itakuwa katika Kushi, watakapoanguka watu waliouawa katika Misri, nao watauondoa wingi wa watu wake, na misingi yake itabomolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vita vitazuka dhidi ya Misri, na wasiwasi mkuu utaikumba nchi ya Kushi, wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa, mali zao zitakapochukuliwa, na misingi ya miji yao kubomolewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Panga zitaingia Misri, nayo nchi ya Nubi itatetemeka, watu waliopigwa kwa panga wakianguka huko Misri, wengine wakizichukua mali zao, tena wakiibomoa misingi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na upanga utakuja juu ya Misri, na dhiki itakuwa katika Kushi, watakapoanguka watu waliouawa katika Misri, nao watauondoa wingi wa watu wake, na misingi yake itabomolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vita itakuja katika inchi ya Misri, na wasiwasi utakuwa katika inchi ya Etiopia, wakati Wamisri wengi wataanguka wameuawa, mali zao zitakaponyanganywa, na misingi ya miji yao kubomolewa.