Ezekiel 30:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wote wanaoiunga mkono Misri wataangamia, mashujaa wake wenye fahari wataangamizwa, tangu Migdoli mpaka Syene watu watauawa vitani. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi; Nao pia wanaoitegemeza Misri wataanguka, na kiburi cha uwezo wake kitashuka; toka Migdoli hata Sewene, wataanguka ndani yake kwa upanga, asema Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wote wanaoiunga mkono Misri wataangamia, mashujaa wake wenye fahari wataangamizwa, tangu Migdoli mpaka Syene watu watauawa vitani. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Hili ndilo BWANA asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Hili ndilo bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi; Nao pia wanaoitegemeza Misri wataanguka, na kiburi cha uwezo wake kitashuka; toka Migdoli hata Sewene, wataanguka ndani yake kwa upanga, asema Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wote wanaoiunga mkono Misri wataangamia, mashujaa wake wenye fahari wataangamizwa, tangu Migdoli mpaka Syene watu watauawa vitani. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nao walioiegemea nchi ya Misri wataangushwa, majivuno ya nguvu zake yakinyenyekezwa; kuanzia Migidoli kufikisha Siwene watauawa kwao kwa panga; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi; Nao pia wanaoitegemeza Misri wataanguka, na kiburi cha uwezo wake kitashuka; toka Migdoli hata Sewene, wataanguka ndani yake kwa upanga, asema Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Wote wanaounga Misri mukono wataangamia, mashujaa wake wenye utukufu wataangamizwa, tangu Migidoli mpaka Sewene watu watauawa katika vita. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.–