Ezekiel 31:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hayo yameupata ili mti wowote ulio mahali penye maji usiweze kurefuka tena kiasi hicho wala kukifikisha kilele chake mawinguni. Mti wowote unaonyweshwa maji usiweze tena kufikia urefu huo. Kwa maana kila kitu mwisho wake ni kifo; hali kadhalika na watu. Wote watashiriki hali yao washukao shimoni kwa wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale wanaoshuka shimoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kusudi mti wo wote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hayo yameupata ili mti wowote ulio mahali penye maji usiweze kurefuka tena kiasi hicho wala kukifikisha kilele chake mawinguni. Mti wowote unaonyweshwa maji usiweze tena kufikia urefu huo. Kwa maana kila kitu mwisho wake ni kifo; hali kadhalika na watu. Wote watashiriki hali yao washukao shimoni kwa wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakaorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani itakayofikia urefu huo, yote mwisho wake ni kifo na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili mti wowote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hayo yameupata ili mti wowote ulio mahali penye maji usiweze kurefuka tena kiasi hicho wala kukifikisha kilele chake mawinguni. Mti wowote unaonyweshwa maji usiweze tena kufikia urefu huo. Kwa maana kila kitu mwisho wake ni kifo; hali kadhalika na watu. Wote watashiriki hali yao washukao shimoni kwa wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa hivyo, kusudi miti yote iliyoko kwenye maji isijikuze, wala isipeleke vilele vyao juu kabisa kupita miti mingine yenye majani mengi, wala ile yenye nguvu isisimame kwa urefu wao na kuishinda yote mingine inyweshwayo, kwani yote imewekewa kufa, ifike mahali palipo chini ya nchi kwenye watu walioshuka shimoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kusudi mti wo wote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hayo yameupata kusudi muti wowote unaokuwa pahali penye maji usiweze kurefuka tena kwa kimo hicho wala kukifikisha kilele chake katika mawingu. Muti wowote unaokunyweshwa maji usiweze tena kufikia urefu huo. Kwa maana kila kitu mwisho wake ni kifo; hata na watu vilevile. Wote watashiriki hali ya wanaoshuka katika shimo kwa wafu.