Ezekiel 31:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miongoni mwa mierezi ya bustanini mwa Mungu, hakuna mti uliolingana nao, wala misonobari haikulingana na matawi yake, mibambakofi haikuwa na matawi kama yake, hata mti wowote wa bustani ya Mungu haukulingana nao kwa uzuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kushindana nao, wala misunobari haikuweza kulingana na vitawi vyake, wala miaramoni haikulinganishwa na matawi yake, wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu wa kulinganisha na uzuri wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mierezi ya bustani ya Mungu haikuweza kumficha; misunobari haikuwa kama vitanzu vyake, na miamori haikuwa kama matawi yake, wala bustanini mwa Mungu hamkuwa na mti wo wote uliofanana naye kwa uzuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miongoni mwa mierezi ya bustanini mwa Mungu, hakuna mti uliolingana nao, wala misonobari haikulingana na matawi yake, mibambakofi haikuwa na matawi kama yake, hata mti wowote wa bustani ya Mungu haukulingana nao kwa uzuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kushindana nao, wala misonobari haikuweza kulingana na vitawi vyake, wala miti ya miamori haikulinganishwa na matawi yake, wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu wa kulinganisha na uzuri wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kushindana nao, wala misunobari haikuweza kulingana na vitawi vyake, wala miaramoni haikulinganishwa na matawi yake, wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu wa kulinganisha na uzuri wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mierezi ya bustani ya Mungu haikuweza kumficha; misonobari haikuwa kama vitanzu vyake, na miamori haikuwa kama matawi yake, wala bustanini mwa Mungu hamkuwa na mti wowote uliofanana naye kwa uzuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miongoni mwa mierezi ya bustanini mwa Mungu, hakuna mti uliolingana nao, wala misonobari haikulingana na matawi yake, mibambakofi haikuwa na matawi kama yake, hata mti wowote wa bustani ya Mungu haukulingana nao kwa uzuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika bustani ya Mungu haukuwako mwangati ulioupita, wala mivinje haikufanana nao kwa matawi yao, wala migude haikuwa yenye machipuko kama huo; miti yote iliyoko bustanini kwake Mungu haikufanana nao kwa uzuri wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mierezi ya bustani ya Mungu haikuweza kumficha; misunobari haikuwa kama vitanzu vyake, na miamori haikuwa kama matawi yake, wala bustanini mwa Mungu hamkuwa na mti wo wote uliofanana naye kwa uzuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati ya miti ya mierezi ya bustani ya Mungu, hakuna muti uliolingana nao, wala misunobari haikulingana na matawi yake, mibambakofi haikuwa na matawi kama yake, hata muti wowote wa bustani ya Mungu haukulingana nao kwa uzuri.