Ezekiel 32:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wako wengi watauawa kwa mapanga ya mashujaa, watu katili kuliko mataifa yote. Watakomesha kiburi cha Misri na kuwaua watu wako wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitayafanya makundi yako kuanguka kwa panga za mashujaa: taifa katili kuliko mataifa yote. Watakivunjavunja kiburi cha Misri, nayo makundi yake yote yatashindwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa panga za mashujaa nitawaangusha watu wako wote jamii; hao wote ni watu wa mataifa watishao, nao watakiharibu kiburi cha Misri, na jamii ya watu wake wengi wataangamia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wako wengi watauawa kwa mapanga ya mashujaa, watu katili kuliko mataifa yote. Watakomesha kiburi cha Misri na kuwaua watu wako wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka kwa panga za watu mashujaa, taifa katili kuliko mataifa yote. Watakivunjavunja kiburi cha Misri, nayo makundi yake yote ya wajeuri yatashindwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka kwa panga za watu mashujaa, taifa katili kuliko mataifa yote. Watakivunjavunja kiburi cha Misri, nayo makundi yake yote ya wajeuri yatashindwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa panga za mashujaa nitawaangusha watu wako umati wote; hao wote ni watu wa mataifa watishao, nao watakiharibu kiburi cha Misri, na jamii ya watu wake wengi wataangamia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wako wengi watauawa kwa mapanga ya mashujaa, watu katili kuliko mataifa yote. Watakomesha kiburi cha Misri na kuwaua watu wako wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa panga za wapiga vita wenye nguvu nitawaua watu wako, ingawa wawe wengi, kwani wale wote ndio wakali kuliko mataifa mengine; watayapoteza majivuno ya Wamisri, watu wao walio wengi watakapoangamizwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa panga za mashujaa nitawaangusha watu wako wote jamii; hao wote ni watu wa mataifa watishao, nao watakiharibu kiburi cha Misri, na jamii ya watu wake wengi wataangamia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wako wengi watauawa kwa mapanga ya mashujaa, watu wa hatari kuliko mataifa yote. Watakomesha kiburi cha Misri na kuwaua watu wako wote.