Ezekiel 32:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Huo ndio utenzi wa maombolezo, wanawake wa mataifa watauimba, wataimba juu ya Misri na watu wake wote. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote wataliimba, asema Bwana Mungu Mwenyezi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hayo ndiyo maombolezo watakayoomboleza; binti za mataifa wataomboleza kwa hayo; kwa hayo wataomboleza kwa ajili ya Misri, na kwa ajili ya watu wake wote jamii, asema Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Huo ndio utenzi wa maombolezo, wanawake wa mataifa watauimba, wataimba juu ya Misri na watu wake wote. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema BWANA Mwenyezi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema bwana Mwenyezi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hayo ndiyo maombolezo watakayoimba; binti za mataifa watayaimba; kwa hayo wataomboleza kwa ajili ya Misri, na kwa ajili ya watu wake umati wote, asema Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Huo ndio utenzi wa maombolezo, wanawake wa mataifa watauimba, wataimba juu ya Misri na watu wake wote. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili ndilo ombolezo la kuimba kwa kuomboleza; wanawali wa mataifa waliimbe kwa kuiombolezea nchi ya Misri, nao watu wake wengi watawaombolezea hivyo; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hayo ndiyo maombolezo watakayoomboleza; binti za mataifa wataomboleza kwa hayo; kwa hayo wataomboleza kwa ajili ya Misri, na kwa ajili ya watu wake wote jamii, asema Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huo ndio wimbo wa maombolezo, wanawake wa mataifa watauimba, wataimba juu ya Misri na watu wake wote. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.