Ezekiel 32:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe mtu! Imba utenzi wa kuomboleza juu ya Farao, mfalme wa Misri. Wewe Farao unajiona kuwa simba kati ya mataifa, lakini wewe ni kama mamba tu majini: Unachomoka kwa nguvu kwenye mito yako, wayavuruga maji kwa miguu yako, na kuichafua mito.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie: “ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa, wewe ni kama mnyama mkubwa baharini, unapiga maji kwa kishindo katika vijito vyako, unayavuruga maji kwa miguu yako, na kuchafua vijito.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwana-simba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe mtu! Imba utenzi wa kuomboleza juu ya Farao, mfalme wa Misri. Wewe Farao unajiona kuwa simba kati ya mataifa, lakini wewe ni kama mamba tu majini: unachomoka kwa nguvu kwenye mito yako, wayavuruga maji kwa miguu yako, na kuichafua mito.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie: “ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa, wewe ni kama joka kubwa baharini, unayevuruga maji kwa miguu yako na kuchafua vijito.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie: “ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa, wewe ni kama joka kubwa baharini, unayevuruga maji kwa miguu yako na kuchafua vijito.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe mtu! Imba utenzi wa kuomboleza juu ya Farao, mfalme wa Misri. Wewe Farao unajiona kuwa simba kati ya mataifa, lakini wewe ni kama mamba tu majini: Unachomoka kwa nguvu kwenye mito yako, wayavuruga maji kwa miguu yako, na kuichafua mito.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu, mtungie Farao, mfalme wa Misri, ombolezo la kwamba: Ulifananishwa na mwana wa simba alioko kwenye mataifa, nawe ulikuwa kama mamba aliomo kwenye maji mengi, mara kwa mara ulitokea kwa nguvu katika mito yako, ukachafua maji kwa miguu yako na kuivurugavuruga mito yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwana-simba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe mwanadamu! Imba wimbo wa kuomboleza juu ya Mufalme wa Misri. Wewe Mufalme wa Misri unajiona kuwa simba kati ya mataifa, lakini wewe ni kama mamba tu katika maji: unachomoka kwa nguvu kwenye mito yako, unayavuruga maji kwa miguu yako, na kuichafua mito.