Ezekiel 32:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Waelamu pia wako huko, wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wao waliouawa vitani. Wote hao wasiomjua Mungu walishuka kwenye nchi ya wafu. Walipokuwa wanaishi bado walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai. Lakini sasa wanabeba aibu yao pamoja na wanaoshuka shimoni kwa wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka Kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Elamu yuko huko, na watu wake wote jamii, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka hali hawana tohara hata pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Waelamu pia wako huko, wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wao waliouawa vitani. Wote hao wasiomjua Mungu walishuka kwenye nchi ya wafu. Walipokuwa wanaishi bado walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai. Lakini sasa wanabeba aibu yao pamoja na wanaoshuka shimoni kwa wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Elamu yuko huko, na watu wake umati wote, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka wakiwa hawajatahiriwa hadi pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Waelamu pia wako huko, wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wao waliouawa vitani. Wote hao wasiomjua Mungu walishuka kwenye nchi ya wafu. Walipokuwa wanaishi bado walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai. Lakini sasa wanabeba aibu yao pamoja na wanaoshuka shimoni kwa wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako Waelamu nao watu wao wengi; wanalizunguka kaburi lake; hao wote wamekufa kwa kuumia wakiangushwa kwa panga, wameshuka pasipo kutahiriwa mahali palipo chini ya nchi; nao ndio waliostusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai, sasa wanashikwa na soni kwao walioshuka shimoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Elamu yuko huko, na watu wake wote jamii, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka hali hawana tohara hata pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elamu nayo iko huko. Makaburi ya waaskari wake yanaizunguka. Wote waliuawa katika vita. Wakashuka kwenye inchi ya wafu, bila kujua Mungu. Walipokuwa wangali wanaishi, walieneza vitisho vyao katika inchi ya wanaokuwa wazima. Lakini sasa wanapata haya yao pamoja na wale wanaoshuka katika shimo kwa wafu.