Ezekiel 32:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wamelazwa na jeshi lao miongoni mwa wale waliouawa vitani. Wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wake wote waliouawa vitani na ambao wote hawamjui Mungu. Walipokuwa bado wanaishi walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai, na sasa wako hapo wamejaa aibu pamoja na wale waliouawa vitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wamemwekea kitanda kati ya hao waliouawa, pamoja na watu wake wote jamii; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana maogofyo yao yalifanyika katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni; amewekwa kati ya hao waliouawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wamelazwa na jeshi lao miongoni mwa wale waliouawa vitani. Wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wake wote waliouawa vitani na ambao wote hawamjui Mungu. Walipokuwa bado wanaishi walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai, na sasa wako hapo wamejaa aibu pamoja na wale waliouawa vitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wamemwekea kitanda kati ya hao waliouawa, pamoja na watu wake umati wote; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana vitisho vyao vilifanyika katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni; amewekwa kati ya hao waliouawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wamelazwa na jeshi lao miongoni mwa wale waliouawa vitani. Wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wake wote waliouawa vitani na ambao wote hawamjui Mungu. Walipokuwa bado wanaishi walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai, na sasa wako hapo wamejaa aibu pamoja na wale waliouawa vitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katikati yao waliouawa kwa panga wamewapa pa kulala penye watu wao wengi, nayo makaburi yao hawa yanawazunguka wenyewe. Wote ni watu wasiotahiriwa waliouawa kwa panga, kwani walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai, lakini sasa wanashikwa na soni kwao walioshuka shimoni, katikati yao waliouawa kwa panga wamepata mahali pao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wamemwekea kitanda kati ya hao waliouawa, pamoja na watu wake wote jamii; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana maogofyo yao yalifanyika katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni; amewekwa kati ya hao waliouawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elamu imelalishwa kati ya wale waliouawa katika vita. Makaburi yao yanaizunguka. Wote waliuawa katika vita, bila kujua Mungu. Walipokuwa wangali wanaishi, walieneza vitisho vyao katika inchi ya wanaokuwa wazima, na sasa wako wanapata haya yao pamoja na wale wanaoshuka katika shimo kwa wafu. Wanawekwa kati ya wale waliouawa.