Ezekiel 32:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu wa Mesheki na wa Tabali wote wako huko, wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wao. Watu hao wote wasiomjua Mungu walikufa vitani, watu ambao walipokuwa hai walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mesheki yuko huko, na Tubali, na watu wake wote jamii; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana walifanya utisho wao katika nchi ya walio hai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu wa Mesheki na wa Tabali wote wako huko, wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wao. Watu hao wote wasiomjua Mungu walikufa vitani, watu ambao walipokuwa hai walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mesheki yuko huko, na Tubali, na watu wake umati wote; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana walitisha katika nchi ya walio hai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu wa Mesheki na wa Tabali wote wako huko, wamezungukwa na makaburi ya wanajeshi wao. Watu hao wote wasiomjua Mungu walikufa vitani, watu ambao walipokuwa hai walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako Wameseki na Watubali nao watu wao wengi, makaburi yao hawa yanawazunguka wenyewe; hawa wote ni watu wasiotahiriwa, walikufa wakiumia kwa panga; kwani walistusha watu walipokuwa katika nchi yao walio hai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mesheki yuko huko, na Tubali, na watu wake wote jamii; makaburi yake yamzunguka; wote pia hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga; maana walifanya utisho wao katika nchi ya walio hai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mesaki na Tubali ziko huko. Makaburi ya watu wake wote yanazizunguka. Wote waliuawa katika vita, bila kujua Mungu. Walipokuwa wangali wanaishi, walieneza vitisho vyao katika inchi ya wanaokuwa wazima.