Ezekiel 32:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Waedomu wako huko pamoja na wafalme wao na wakuu wao wote. Walipokuwa bado hai walikuwa na nguvu sana, lakini sasa wamelazwa kwa wafu pamoja na wasiomjua Mungu waliouawa vitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale wanaoshuka shimoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Edomu yuko huko, wafalme wake, na wakuu wake wote, ambao katika uwezo wao wamelazwa pamoja nao waliouawa kwa upanga; watalala pamoja na hao wasiotahiriwa, na pamoja na hao washukao shimoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Waedomu wako huko pamoja na wafalme wao na wakuu wao wote. Walipokuwa bado hai walikuwa na nguvu sana, lakini sasa wamelazwa kwa wafu pamoja na wasiomjua Mungu waliouawa vitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Edomu yuko huko, wafalme wake, na wakuu wake wote, ambao katika uwezo wao wamelazwa pamoja nao waliouawa kwa upanga; watalala pamoja na hao wasiotahiriwa, na pamoja na hao washukao shimoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Waedomu wako huko pamoja na wafalme wao na wakuu wao wote. Walipokuwa bado hai walikuwa na nguvu sana, lakini sasa wamelazwa kwa wafu pamoja na wasiomjua Mungu waliouawa vitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako Waedomu, wafalme wao na wakuu wao, waliokuwa wenye nguvu za kupiga vita, lakini nao wamepewa mahali pao kwao waliokufa wakiumia kwa panga, walale nao kwao wasiotahiriwa walioshuka shimoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Edomu yuko huko, wafalme wake, na wakuu wake wote, ambao katika uwezo wao wamelazwa pamoja nao waliouawa kwa upanga; watalala pamoja na hao wasiotahiriwa, na pamoja na hao washukao shimoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Edomu iko huko pamoja na wafalme wake na wakubwa wao wote. Walipokuwa wangali wanaishi walikuwa na nguvu sana, lakini sasa wamelalishwa kwa wafu pamoja na wasiomujua Mungu waliouawa katika vita.