Ezekiel 32:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Viongozi wote wa watu wa kaskazini wako huko pia; hata Wasidoni wote walikwenda kujiunga na wafu. Walipokuwa bado wanaishi, walisababisha vitisho kwa nguvu zao, lakini sasa hao wasiomjua Mungu wamelazwa chini kwa aibu pamoja na wale waliouawa vitani. Wanashiriki aibu ya wale walioshuka shimoni kwa wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakuu wa kaskazini wako huko, wote pia, na Wasidoni, wote walioshuka pamoja na hao waliouawa; kwa sababu ya utisho walioufanya katika uwezo wao wamefedheheka, nao wamelala hali hawana tohara, pamoja nao waliouawa kwa upanga, nao wanachukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Viongozi wote wa watu wa kaskazini wako huko pia; hata Wasidoni wote walikwenda kujiunga na wafu. Walipokuwa bado wanaishi, walisababisha vitisho kwa nguvu zao, lakini sasa hao wasiomjua Mungu wamelazwa chini kwa aibu pamoja na wale waliouawa vitani. Wanashiriki aibu ya wale walioshuka shimoni kwa wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakuu wa kaskazini wako huko, wote pia, na Wasidoni, wote walioshuka pamoja na hao waliouawa; kwa sababu ya hofu waliyoleta katika uwezo wao wamefedheheka, nao wamelala wakiwa hawajatahiriwa, pamoja nao waliouawa kwa upanga, nao wanachukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Viongozi wote wa watu wa kaskazini wako huko pia; hata Wasidoni wote walikwenda kujiunga na wafu. Walipokuwa bado wanaishi, walisababisha vitisho kwa nguvu zao, lakini sasa hao wasiomjua Mungu wamelazwa chini kwa aibu pamoja na wale waliouawa vitani. Wanashiriki aibu ya wale walioshuka shimoni kwa wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako wakuu wa kaskazini wote pamoja na Wasidoni wote walioshuka kwao waliokufa wakiumia kwa panga; walikuwa wakistusha watu kwa nguvu zao za kupiga vita, lakini soni za kushindwa zikawapata nao, sasa wanalala pasipo kutahiriwa kwao waliokufa wakiumia kwa panga wakishikwa na soni kwao walioshuka shimoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakuu wa kaskazini wako huko, wote pia, na Wasidoni, wote walioshuka pamoja na hao waliouawa; kwa sababu ya utisho walioufanya katika uwezo wao wamefedheheka, nao wamelala hali hawana tohara, pamoja nao waliouawa kwa upanga, nao wanachukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wote wa watu wa upande wa kaskazini wako huko vilevile; hata Wasidoni wote walikwenda kujiunga na wafu. Walipokuwa wangali wanaishi, walisababisha vitisho kwa nguvu zao, lakini sasa hao wasiomujua Mungu wamelalishwa chini na haya pamoja na wale waliouawa katika vita. Wanashiriki haya ya wale walioshuka ndani ya shimo kwa wafu.