Ezekiel 33:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi namwahidi mwadilifu kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba uadilifu wake watosha, akaanza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya hapo awali hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika ataishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa; atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi namwahidi mwadilifu kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba uadilifu wake watosha, akaanza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya hapo awali hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lo lote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Japo ninapomwambia mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akitenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi namwahidi mwadilifu kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba uadilifu wake watosha, akaanza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya hapo awali hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikimwambia mwongofu, ya kuwa atapata uzima, naye akiuegemea wongofu wake, afanye mapotovu, basi, wongofu wake wote hautakumbukwa tena, naye atakufa kwa ajili ya hayo mapotovu, aliyoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ninamwahidi mutu wa haki kwamba ataishi; lakini yeye akiamini kwamba haki yake inatosha, akianza kutenda uovu, matendo yake yote mema ya zamani hayatakumbukwa; atakufa kwa uovu wake.