Ezekiel 33:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi mnakula nyama yenye damu, mnaziabudu sanamu za miungu yenu na kuua! Je, mnadhani mtapewa nchi hii iwe yenu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa kuwa mnakula nyama ikiwa na damu, na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Mnakula nyama pamoja na damu yake, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi mnakula nyama yenye damu, mnaziabudu sanamu za miungu yenu na kuua! Je, mnadhani mtapewa nchi hii iwe yenu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa mnakula nyama pamoja na damu na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa mnakula nyama pamoja na damu na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Mnakula nyama pamoja na damu yake, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi mnakula nyama yenye damu, mnaziabudu sanamu za miungu yenu na kuua! Je, mnadhani mtapewa nchi hii iwe yenu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ninyi hula nyama zenye damu, tena huyaelekezea magogo yenu ya kutambikia macho yenu, tena humwaga damu za watu! Je? Hivyo mtaipata nchi hii, iwe yenu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Mnakula nyama pamoja na damu yake, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, uwaambie kwamba Bwana wetu Yawe anasema hivi: Ninyi munakula nyama yenye damu, munaziabudu sanamu za miungu yenu na kumwanga damu! Munazani kwamba mutapewa inchi hii ikuwe yenu?