Ezekiel 33:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivi ndivyo utakavyowaambia, Bwana MUNGU asema hivi; Kama mimi niishivyo, hakika watu wale wakaao mahali palipoharibika wataanguka kwa upanga, naye mtu aliye katika uwanda, nitamtoa na kuwapa wanyama wakali, ili aliwe; na hao walio ndani ya ngome na mapango watakufa kwa tauni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Waambie hivi: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Waambie hivi: ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivi ndivyo utakavyowaambia, Bwana MUNGU asema hivi; Kama mimi niishivyo, hakika watu wale wakaao mahali palipoharibika wataanguka kwa upanga, naye mtu aliye katika uwanda, nitamtoa na kuwapa wanyama wakali, ili aliwe; na hao walio ndani ya ngome na mapango watakufa kwa tauni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kama niishivyo mimi naapa kwamba hao wanaokaa katika miji hiyo iliyo magofu, wataangamia kwa upanga; aliye uwanjani nitamtoa aliwe na wanyama wakali; na wale walio ndani ya ngome na mapangoni watakufa kwa maradhi mabaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti uwaambie hivi: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, wayakaliao yale mabomoko watauawa kwa panga, nao walioko shambani nitawatoa, waliwe na nyama wa porini, nao walioko vilimani ngomeni na mapangoni watakufa kwa magonjwa mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivi ndivyo utakavyowaambia, Bwana MUNGU asema hivi; Kama mimi niishivyo, hakika watu wale wakaao mahali palipoharibika wataanguka kwa upanga, naye mtu aliye katika uwanda, nitamtoa na kuwapa wanyama wakali, ili aliwe; na hao walio ndani ya ngome na mapango watakufa kwa tauni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie hivi: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Kama vile ninavyoishi, hao wanaokaa katika miji hiyo inayokuwa mabomoko, wataagamia kwa upanga; anayekuwa katika vijiji nitamutoa akuliwe na nyama wakali; na wale wanaokuwa kwa milima na ndani ya mapango watakufa kwa ugonjwa mukali.