Ezekiel 33:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Wananchi wenzako wanazungumza juu yako, wameketi kutani na milangoni mwa nyumba zao na kuambiana: ‘Haya! Twende tukasikie neno alilosema Mwenyezi-Mungu!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule unaotoka kwa Mwenyezi Mungu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe, mwanadamu, wana wa watu wako husimulia habari zako karibu na kuta, na ndani ya milango ya nyumba zao, na kuambiana, kila mtu na ndugu yake, wakisema, Haya! Twende tukasikie ni neno gani hilo litokalo kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Wananchi wenzako wanazungumza juu yako, wameketi kutani na milangoni mwa nyumba zao na kuambiana: ‘Haya! Twende tukasikie neno alilosema Mwenyezi-Mungu!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njoni msikie ujumbe ule utokao kwa BWANA.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule utokao kwa bwana.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe, mwanadamu, wana wa watu wako husimulia habari zako karibu na kuta, na ndani ya milango ya nyumba zao, na kuambiana, kila mtu na ndugu yake, wakisema, Haya! Twende tukasikie ni neno gani hilo litokalo kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliniambia, “Wewe mtu! Wananchi wenzako wanazungumza juu yako, wameketi kutani na milangoni mwa nyumba zao na kuambiana: ‘Haya! Twende tukasikie neno alilosema Mwenyezi-Mungu!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe mwana wa mtu, wana wao walio ukoo wako huzisimulia habari za kwako barazani namo milangoni mwa nyumba, husemezana kila mmoja na mwenziwe, kila mtu na ndugu yake kwamba: Njoni, msikie, kama ni neno gani lililotoka kwake Bwana!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe, mwanadamu, wana wa watu wako husimulia habari zako karibu na kuta, na ndani ya milango ya nyumba zao, na kuambiana, kila mtu na ndugu yake, wakisema, Haya! Twende tukasikie ni neno gani hilo litokalo kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliniambia: Wewe mwanadamu! Wanainchi wenzako wanasema juu yako, wameikaa juu ya kuta na kwenye milango ya nyumba zao na kuambiana: Tuende kusikiliza neno Yawe alilosema!