Ezekiel 34:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawapa malisho mazuri kwenye milima mirefu ya Israeli ambako yako malisho yao. Watapumzika huko kwenye mbuga za malisho mazuri; naam, watapata malisho mazuri juu ya milima ya Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima ya mahali palipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawapa malisho mazuri kwenye milima mirefu ya Israeli ambako yako malisho yao. Watapumzika huko kwenye mbuga za malisho mazuri; naam, watapata malisho mazuri juu ya milima ya Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha kwa amani katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha kwa amani katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima ya mahali palipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawapa malisho mazuri kwenye milima mirefu ya Israeli ambako yako malisho yao. Watapumzika huko kwenye mbuga za malisho mazuri; naam, watapata malisho mazuri juu ya milima ya Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawachunga penye malisho mema, tena mazizi yao yatakuwa juu ya milima mirefu ya Waisiraeli; huko watalala katika mazizi mema, wakilisha malisho ya kuwanonesha katika milima ya Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima ya mahali palipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawapa malisho mazuri kwenye milima mirefu ya inchi ya Israeli ambako kuna mashamba mazuri ya kuwakulishia. Watapumzika huko kwenye mbuga za malisho mazuri; watapata malisho mazuri juu ya milima ya inchi ya Israeli.