Ezekiel 34:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kondoo waliopotea nitawatafuta na waliotangatanga nitawarudisha nyumbani. Waliojeruhiwa nitawatibu, na wale walio dhaifu nitawapa nguvu. Kondoo wanono na wenye nguvu nitawaangamiza. Mimi nitawachunga kondoo kama itakiwavyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta waliotangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu walio dhaifu, lakini wale walionona na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kondoo waliopotea nitawatafuta na waliotangatanga nitawarudisha nyumbani. Waliojeruhiwa nitawatibu, na wale walio dhaifu nitawapa nguvu. Kondoo wanono na wenye nguvu nitawaangamiza. Mimi nitawachunga kondoo kama itakiwavyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta walio tangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu waliodhaifu lakini wale waliojikinai na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta waliotangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu walio dhaifu lakini wale waliojikinai na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliotangatanga, nitawatibu waliojeruhiwa, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kondoo waliopotea nitawatafuta na waliotangatanga nitawarudisha nyumbani. Waliojeruhiwa nitawatibu, na wale walio dhaifu nitawapa nguvu. Kondoo wanono na wenye nguvu nitawaangamiza. Mimi nitawachunga kondoo kama itakiwavyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waliopotea nitawatafuta, nao waliokimbizwakimbizwa nitawarudisha, nao waliovunjika nitawafunga vitambaa, nao waliougua nitawatia nguvu; lakini wenye mafuta na wenye nguvu nitawaangamiza, niwachunge na kuwapatiliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawatafuta kondoo waliopotea na waliotangatanga nitawarudisha kwa nyumba. Waliovunjika nitawatunza, na wale wanaokuwa zaifu nitawapatia nguvu. Lakini kondoo wanono na wenye nguvu nitawaangamiza. Mimi nitawachunga kondoo kama inavyostahili.