Ezekiel 34:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nitawafanya waishi kandokando ya mlima wangu mtakatifu na kuwabariki. Nitawaletea mvua kwa wakati wake, nazo zitakuwa mvua za baraka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwa na mvua za baraka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nitawafanya waishi kandokando ya mlima wangu mtakatifu na kuwabariki. Nitawaletea mvua kwa wakati wake, nazo zitakuwa mvua za baraka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nitawafanya waishi kandokando ya mlima wangu mtakatifu na kuwabariki. Nitawaletea mvua kwa wakati wake, nazo zitakuwa mvua za baraka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawapatia mbaraka wao wenyewe nazo nchi zangu zenye vilima ziwazungukazo, nikizinywesha mvua, siku zake zitakapotimia; nazo hizo mvua zitakuwa mvua zenye mbaraka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawafanya waishi kandokando ya mulima wangu mutakatifu na kuwabariki. Nitawaletea mvua kwa wakati wake, nazo zitakuwa mvua za baraka.