Ezekiel 34:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miti mashambani itazaa matunda, ardhi itatoa mazao kwa wingi, nao wataishi salama katika nchi yao. Nitakapovunja nira zao za utumwa na kuwaokoa mikononi mwa hao waliowafanya kuwa watumwa ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka mikono ya wale waliowafanya watumwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mti wa kondeni utazaa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya kongwa lao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale waliowatumikisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miti mashambani itazaa matunda, ardhi itatoa mazao kwa wingi, nao wataishi salama katika nchi yao. Nitakapovunja nira zao za utumwa na kuwaokoa mikononi mwa hao waliowafanya kuwa watumwa ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimi BWANA, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka katika mikono ya wale waliowafanya watumwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimi bwana, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka mikono ya wale waliowafanya watumwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mti wa kondeni utazaa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapovunja vifungo vya nira zao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale waliowatumikisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miti mashambani itazaa matunda, ardhi itatoa mazao kwa wingi, nao wataishi salama katika nchi yao. Nitakapovunja nira zao za utumwa na kuwaokoa mikononi mwa hao waliowafanya kuwa watumwa ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miti ya shambani itazaa matunda yao, nayo nchi itawapa mazao yake, watakaa katika nchi yao; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapoivunja miti ya makongwa yao na kuwaopoa mikononi mwao waliowatumikisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mti wa kondeni utazaa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapovunja vifungo vya kongwa lao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale waliowatumikisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Miti inayokuwa katika mashamba itazaa matunda, udongo utatoa mazao kwa wingi, nao wataishi kwa salama katika inchi yao. Nitakapovunja nira zao za utumwa na kuwaokoa toka katika mikono ya hao waliowafanya kuwa watumwa halafu watatambua kwamba mimi ni Yawe.