Ezekiel 34:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, kondoo wangu walitawanywa, wakatangatanga milimani na vilimani. Kondoo walisambazwa duniani kote, na hapakuwa na mtu aliyejali juu yao wala kuwatafuta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kondoo wangu walitangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika duniani kote, bila yeyote wa kuwaulizia wala kuwatafuta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kondoo zangu walitanga-tanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo zangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, kondoo wangu walitawanywa, wakatangatanga milimani na vilimani. Kondoo walisambazwa duniani kote, na hapakuwa na mtu aliyejali juu yao wala kuwatafuta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na ye yote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na yeyote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kondoo wangu walitangatanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, kondoo wangu walitawanywa, wakatangatanga milimani na vilimani. Kondoo walisambazwa duniani kote, na hapakuwa na mtu aliyejali juu yao wala kuwatafuta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kondoo wangu wakatangatanga milimani po pote napo po pote penye vilima vinavyokwenda juu; ikawa hivyo, kondoo wangu wakitawanyika katika nchi yote nzima, lakini hakuwako wala aliyewauliza, kama wako wapi, wala aliyewatafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kondoo zangu walitanga-tanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo zangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli, kondoo walisambazwa, wakatangatanga juu ya milima na vilima. Kondoo walisambazwa katika dunia yote, na hakukukuwa mutu aliyejali juu yao wala kuwatafuta.