Ezekiel 34:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, naapa kwamba: Nimechoka kuwaona kondoo wangu wamekuwa mawindo ya wanyama wakali kwa vile hapakuwa na mchungaji; wachungaji wangu hawakuwatafuta kondoo wangu, bali wamejilisha wao wenyewe badala ya kuwalisha kondoo wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, kwa sababu kondoo wangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama pori wote na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo wangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo wangu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo zangu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, naapa kwamba: nimechoka kuwaona kondoo wangu wamekuwa mawindo ya wanyama wakali kwa vile hapakuwa na mchungaji; wachungaji wangu hawakuwatafuta kondoo wangu, bali wamejilisha wao wenyewe badala ya kuwalisha kondoo wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hakika kama niishivyo, asema BWANA Mwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hakika kama niishivyo, asema bwana Mwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo wangu walikuwa mateka, kondoo wangu wakawa chakula cha wanyamamwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo wangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo wangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, naapa kwamba: Nimechoka kuwaona kondoo wangu wamekuwa mawindo ya wanyama wakali kwa vile hapakuwa na mchungaji; wachungaji wangu hawakuwatafuta kondoo wangu, bali wamejilisha wao wenyewe badala ya kuwalisha kondoo wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, kweli kondoo wangu wamepokonywa, kondoo wangu wakawa chakula cha nyama wote wa porini, kwa kuwa hawana mchungaji, kwa kuwa wachungaji wangu hawakuwatafuta kondoo wangu, wakajichunga wenyewe, wasiwachunge kondoo wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo zangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile ninavyoishi, –ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe– nimechoka kuwaona kondoo wangu wamekuwa chakula cha nyama wakali kwa vile hakukukuwa muchungaji; wachungaji wangu hawakuwatafuta kondoo wangu, lakini wamejikulisha wao wenyewe pahali pa kuwakulisha kondoo wangu.