Ezekiel 35:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe ulisema ya kwamba mataifa hayo mawili yaani Yuda na Israeli ni mali yako na kwamba utazimiliki! Ulisema hivyo ingawa humo ni makao yangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata Mimi Mwenyezi Mungu nilikuwa huko,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa Bwana alikuwako huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe ulisema ya kwamba mataifa hayo mawili yaani Yuda na Israeli ni mali yako na kwamba utazimiliki! Ulisema hivyo ingawa humo ni makao yangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata mimi BWANA nilikuwa huko,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata mimi bwana nilikuwa huko,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa BWANA alikuwako huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe ulisema ya kwamba mataifa hayo mawili yaani Yuda na Israeli ni mali yako na kwamba utazimiliki! Ulisema hivyo ingawa humo ni makao yangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa ulisema: Hayo mataifa mawili nazo nchi zao mbili zitakuwa zangu, tuzichukue! naye Bwama alikuwa yupo;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa BWANA alikuwako huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe ulisema kwamba mataifa hayo mawili, ni kusema inchi ya Yuda na ya Israeli, ni mali yako na kwamba utazirizi! Ulisema hivyo ingawa humo ni makao yangu mimi Yawe.