Ezekiel 35:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe utajua ya kwamba mimi mwenyewe Mwenyezi-Mungu nimeyasikia matusi yote uliyoyatoa dhidi ya milima ya Israeli, ukisema: ‘Milima ya Israeli imefanywa kuwa jangwa! Tumepewa sisi tuinyakue!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo utakapojua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utajua ya kuwa mimi, Bwana, nimeyasikia matukano yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe utajua ya kwamba mimi mwenyewe Mwenyezi-Mungu nimeyasikia matusi yote uliyoyatoa dhidi ya milima ya Israeli, ukisema: ‘Milima ya Israeli imefanywa kuwa jangwa! Tumepewa sisi tuinyakue!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo utakapojua kuwa Mimi BWANA nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo utakapojua kuwa Mimi bwana nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeyasikia matusi yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe utajua ya kwamba mimi mwenyewe Mwenyezi-Mungu nimeyasikia matusi yote uliyoyatoa dhidi ya milima ya Israeli, ukisema: ‘Milima ya Israeli imefanywa kuwa jangwa! Tumepewa sisi tuinyakue!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, utakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana. Nimeyasikia maapizo yako yote, uliyoyasema na kuiapiza milima ya Isiraeli kwamba: Na iwe mapori, tupewe sisi kuila!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeyasikia matukano yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe utajua kwamba mimi mwenyewe Yawe nimeyasikia matusi yote uliyoyatoa juu ya milima ya Waisraeli, ukisema: Milima ya Israeli imefanywa kuwa jangwa! Imetolewa kusudi tupate kuinyanganya!