Ezekiel 36:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe mtu! Waisraeli walipoishi katika nchi yao waliitia unajisi kwa mienendo na matendo yao. Niliyaona matendo yao kuwa sawa na mwanamke aliye najisi wakati wa siku zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe mtu! Waisraeli walipoishi katika nchi yao waliitia unajisi kwa mienendo na matendo yao. Niliyaona matendo yao kuwa sawa na mwanamke aliye najisi wakati wa siku zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe mtu! Waisraeli walipoishi katika nchi yao waliitia unajisi kwa mienendo na matendo yao. Niliyaona matendo yao kuwa sawa na mwanamke aliye najisi wakati wa siku zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu, walio mlango wa Isiraeli walipokaa katika nchi yao, waliitia uchafu kwa njia zao na kwa matendo yao; njia zao zilikuwa machoni pangu kama uchafu wa mwanamke mwenye siku zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe mwanadamu! Waisraeli walipoishi katika inchi yao waliichafua kwa mienendo na matendo yao. Niliyaona matendo yao kuwa sawa na mwanamuke anayekuwa muchafu wakati wa ugonjwa wake wa mwezi.