Ezekiel 36:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwatawanya kati ya mataifa, wakasambazwa katika nchi nyingine. Niliwaadhibu kadiri ya tabia yao na matendo yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakatapanywa katika nchi mbalimbali; nikawahukumu kulingana na mwenendo wao na matendo yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikawatawanya katika mataifa, wakatapanyika katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao, naliwahukumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwatawanya kati ya mataifa, wakasambazwa katika nchi nyingine. Niliwaadhibu kadiri ya tabia yao na matendo yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakaenda huko na huko katika nchi mbalimbali, nikawahukumu sawasawa na mwenendo wao na matendo yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakaenda huku na huko katika nchi mbalimbali, nikawahukumu sawasawa na mwenendo wao na matendo yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikawatawanya katika mataifa, wakasambaa katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao, niliwahukumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwatawanya kati ya mataifa, wakasambazwa katika nchi nyingine. Niliwaadhibu kadiri ya tabia yao na matendo yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawatawanya kwenye wamizimu na kuwatupatupa katika hizo nchi zao nilipowahukumu kwa hivyo, njia zao na matendo yao yalivyokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikawatawanya katika mataifa, wakatapanyika katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao, naliwahukumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwasambaza kati ya mataifa, wakasambazwa katika inchi nyingine. Niliwaazibu kadiri ya tabia yao na matendo yao.