Ezekiel 36:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata walipokuwa miongoni mwa mataifa walilikufuru jina langu takatifu, hata watu wakasema hivi juu yao: ‘Tazama! Hawa ndio wale watu wa Mwenyezi-Mungu, lakini wamelazimika kuondoka katika nchi yake!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tena popote walipoenda miongoni mwa mataifa walilinajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuwahusu, ‘Hawa ndio watu wa Mwenyezi Mungu, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipoyafikilia mataifa yale waliyoyaendea, walilitia unajisi jina langu takatifu; kwa kuwa watu waliwanena, wakisema, Watu hawa ni watu wa Bwana, nao wametoka katika nchi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata walipokuwa miongoni mwa mataifa walilikufuru jina langu takatifu, hata watu wakasema hivi juu yao: ‘Tazama! Hawa ndio wale watu wa Mwenyezi-Mungu, lakini wamelazimika kuondoka katika nchi yake!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tena po pote walipokwenda miongoni mwa mataifa walilitia unajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuhusu wao, ‘Hawa ndio watu wa BWANA, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tena popote walipokwenda miongoni mwa mataifa walilitia unajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuwahusu, ‘Hawa ndio watu wa bwana, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipoyafikia mataifa yale waliyoyaendea, walilitia unajisi jina langu takatifu; kwa kuwa watu waliwanena, wakisema, Watu hawa ni watu wa BWANA, nao wametoka katika nchi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata walipokuwa miongoni mwa mataifa walilikufuru jina langu takatifu, hata watu wakasema hivi juu yao: ‘Tazama! Hawa ndio wale watu wa Mwenyezi-Mungu, lakini wamelazimika kuondoka katika nchi yake!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipofika kwenye wamizimu wakalipatia Jina langu takatifu uchafu po pote, walipofika, watu wakisema kwa ajili yao: Hawa ndio walio ukoo wake Bwana, wametolewa katika nchi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipoyafikilia mataifa yale waliyoyaendea, walilitia unajisi jina langu takatifu; kwa kuwa watu waliwanena, wakisema, Watu hawa ni watu wa BWANA, nao wametoka katika nchi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata walipokuwa kati ya mataifa walilikufuru jina langu takatifu, hata watu wakasema hivi juu yao: Hawa ndio wale watu wa Yawe, lakini wamelazimishwa kuondoka katika inchi yake!