Ezekiel 36:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitalirudishia hadhi yake takatifu jina langu kuu mlilokufuru miongoni mwa mataifa. Hapo ndipo mataifa yatakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawatumia nyinyi kuonesha utakatifu wangu mbele yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitauonesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, asema Bwana Mungu Mwenyezi, nitakapojionesha mwenyewe kuwa mtakatifu kupitia kwenu mbele ya macho yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitalitakasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitalirudishia hadhi yake takatifu jina langu kuu mlilokufuru miongoni mwa mataifa. Hapo ndipo mataifa yatakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawatumia nyinyi kuonesha utakatifu wangu mbele yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitauonyesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA, asema BWANA Mwenyezi, nitakapojionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa kuwapitia ninyi mbele ya macho yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitauonyesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watakapojua kuwa Mimi ndimi bwana, asema bwana Mwenyezi, nitakapojionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa kuwapitia ninyi mbele ya macho yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitalitakasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitalirudishia hadhi yake takatifu jina langu kuu mlilokufuru miongoni mwa mataifa. Hapo ndipo mataifa yatakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawatumia nyinyi kuonesha utakatifu wangu mbele yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitalitakasa tena Jina langu kuu lililopatiwa uchafu kwenye wamizimu, mlilolipatia uchafu kwao; ndipo wamizimu watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapotakasika kwenu machoni pao; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitalitakasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitalitakasa jina langu kubwa mulilokufuru kati ya mataifa. Na kwa hiyo mataifa yatatambua kwamba mimi ni Yawe. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.– Nitawatumia ninyi kuonyesha utakatifu wangu mbele yao.