Ezekiel 36:38 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wataniomba wawe wengi kama kundi la kondoo wa tambiko, naam, kama kundi la kondoo mjini Yerusalemu wakati wa sikukuu zake. Hivyo ndivyo miji yenu iliyokuwa ukiwa itakavyojaa makundi ya watu. Hapo ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama kundi lililo tayari kutolewa sadaka, kama kundi la Yerusalemu katika sikukuu zake zilizoamriwa; ndivyo itakavyojazwa watu, miji ile iliyokuwa maganjo; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wataniomba wawe wengi kama kundi la kondoo wa tambiko, naam, kama kundi la kondoo mjini Yerusalemu wakati wa sikukuu zake. Hivyo ndivyo miji yenu iliyokuwa ukiwa itakavyojaa makundi ya watu. Hapo ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama kundi lililo tayari kutolewa sadaka, kama kundi la Yerusalemu katika sikukuu zake zilizoamriwa; ndivyo itakavyojazwa watu, miji ile iliyokuwa maganjo; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wataniomba wawe wengi kama kundi la kondoo wa tambiko, naam, kama kundi la kondoo mjini Yerusalemu wakati wa sikukuu zake. Hivyo ndivyo miji yenu iliyokuwa ukiwa itakavyojaa makundi ya watu. Hapo ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama kondoo wa kutambika walivyo wengi, au kama mle Yerusalemu makundi ya watu yanavyokuwa mengi siku za sikukuu, ndivyo, miji iliyo mabomoko tu itakavyojaa makundi ya watu; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama kundi lililo tayari kutolewa sadaka, kama kundi la Yerusalemu katika sikukuu zake zilizoamriwa; ndivyo itakavyojazwa watu, miji ile iliyokuwa maganjo; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wataniomba wakuwe wengi kama kundi la kondoo wa kutolewa sadaka, kama kundi la kondoo katika Yerusalema wakati wa sikukuu zake. Hivi ndivyo miji yenu iliyokuwa ukiwa itakavyojaa makundi ya watu. Kwa hiyo watatambua kwamba mimi ni Yawe.