Ezekiel 36:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, enyi milima ya Israeli, sikieni neno langu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu: Nyinyi milima na vilima, mifereji na mabonde, nyika tupu na miji mmehamwa, mkatekwa nyara na kudharauliwa na mataifa yote yanayowazungukeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa hiyo, ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana Mungu Mwenyezi: Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa sababu hiyo, enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi hiyo milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, mahali palipoharibika na kuwa ukiwa, na miji iliyoachwa na watu, ambayo imekuwa mateka, na kuzomewa na mabaki ya mataifa, walio karibu pande zote;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, enyi milima ya Israeli, sikieni neno langu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu: Nyinyi milima na vilima, mifereji na mabonde, nyika tupu na miji mmehamwa, mkatekwa nyara na kudharauliwa na mataifa yote yanayowazungukeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa hiyo, Ee milima ya Israeli, sikieni neno la BWANA Mwenyezi: Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa hiyo, ee milima ya Israeli, sikieni neno la bwana Mwenyezi: Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa sababu hiyo, enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi hiyo milima na vilima, mito ya maji na mabonde, mahali palipoharibika na kuwa ukiwa, na miji iliyoachwa na watu, ambayo imekuwa mateka, na kuzomewa na mabaki ya mataifa, walio karibu pande zote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, enyi milima ya Israeli, sikieni neno langu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu: Nyinyi milima na vilima, mifereji na mabonde, nyika tupu na miji mmehamwa, mkatekwa nyara na kudharauliwa na mataifa yote yanayowazungukeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hiyo, ninyi milima ya Isiraeli, sikieni neno la Bwana Mungu: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyoiambia milima iliyo mirefu nayo iliyo mifupi, hata makorongo na mabonde, nayo mabomoko na mapori, nayo miji iliyo mahame tu, iliyonyang'anywa na kuzomelewa na masao ya mataifa yaliyokaa na kuizunguka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa sababu hiyo, enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi hiyo milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, mahali palipoharibika na kuwa ukiwa, na miji iliyoachwa na watu, ambayo imekuwa mateka, na kuzomewa na mabaki ya mataifa, walio karibu pande zote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, enyi milima ya Waisraeli, musikie neno la Bwana wenu Yawe. Anasema juu ya ninyi milima na vilima, mifereji na mabonde, jangwa tupu na miji ya matongo, na miji iliyokamatwa mateka na kuzarauliwa na mataifa yote yanayowazunguka.