Ezekiel 36:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi Bwana MUNGU asema hivi; Hakika kwa moto wa wivu wangu nimenena juu ya mabaki ya mataifa, na juu ya Edomu yote, waliojiandikia nchi yangu kuwa milki yao, kwa furaha ya mioyo yao yote, kwa jeuri ya roho zao, ili waitupe nje kuwa mawindo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi Bwana MUNGU asema hivi; Hakika kwa moto wa wivu wangu nimenena juu ya mabaki ya mataifa, na juu ya Edomu yote, waliojiandalia nchi yangu kuwa milki yao, kwa furaha ya mioyo yao yote, kwa ujeuri wa roho zao, wakatwaa nchi yangu kuwa milki yao, kwa sababu ya malisho yake, ili kuipora;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Kweli itakuwa kwa moto wa wivu wangu, nikisema nao walio masao ya mataifa nao Waedomu wote waliojipa wenyewe nchi yangu, waichukue, iwe yao, wakafurahi kwa mioyo yote na kwa roho zenye mabezo walipowafukuza wa kwenu na kuwanyang'anya mali zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi Bwana MUNGU asema hivi; Hakika kwa moto wa wivu wangu nimenena juu ya mabaki ya mataifa, na juu ya Edomu yote, waliojiandikia nchi yangu kuwa milki yao, kwa furaha ya mioyo yao yote, kwa jeuri ya roho zao, ili waitupe nje kuwa mawindo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana wenu Yawe anasema hivi: Wivu wangu unawaka sana. Nitayaazibu mataifa mengine na hasa watu wa inchi ya Edomu. Wao kwa furaha ndani ya moyo na mazarau walikamata hiyo inchi inayokuwa yangu ikuwe yao.