Ezekiel 36:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi katika kutabiri habari za nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nimenena katika wivu wangu na hasira yangu, kwa sababu mmechukua aibu ya mataifa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi katika kutabiri habari za nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nimenena katika wivu wangu na hasira yangu, kwa sababu mmetukanwa na mataifa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo ifumbulie nchi ya Isiraeli yatakayokuwa ukiiambia milima mirefu na mifupi, nayo makorongo na mabonde: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikisema kwa wivu na kwa makali yangu yenye moto, kwa kuwa mmejitwika yaliyowatia soni kwa wamizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi katika kutabiri habari za nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nimenena katika wivu wangu na hasira yangu, kwa sababu mmechukua aibu ya mataifa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, ewe mwanadamu, toa unabii juu ya inchi ya Waisraeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kwamba Bwana wao Yawe anasema hivi: Ninasema kutokana na upendo wangu wenye wivu juu ya ninyi, inchi yangu, kwa sababu mumetukanwa na watu wa mataifa.